Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Msami Baby amefunguka na kusema kuwa hana tatizo na aliyekuwa mpenzi wake muigizaji wa Bongo Movie, Irene Uwoya licha ya kurushiana maneno katika mitandao ya kijamii.

Kauli hiyo ya Msami inakuja  baada ya siku za hivi karibuni kurushiana mananeo na Irene Uwoya kupitia mtandao wa Instagram baada ya Msami kuposti neno lililosema ‘Eti Ndoa’.

Baada ya kuposti maneno hayo, Irene Uwoya nae akajibu kwa kuposti picha ya msanii huyo na kuandika ‘The best dancer in Africa….usiforce ndiyo kuwa hapana…and plzzzz panic at your own risk’.

Kutokana na maneno ya wasanii hao kumetokea sintofahamu kwa mashabiki wa wasanii hao kutaka kufahamu nini kinaendelea kati yao.

Msami na Irene Uwoya walishawahi kuwa Kwenye Mahusiano ya kimapenzi miaka ya nyuma kabla ya kuachana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *