Mrembo, Julietha Kabete anaiwakilisha Tanzania katika mashindano ya urembo Bara la Afrika kwa mwaka 2016 yatakayofanyika nchini Nigeria Novemba 28 mwaka huu nchini Nigeria.

Julietha Kabete ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuunga mkono mashindano mbalimbali ya urembo Tanzania inaposhiriki.

Mwakilishi wa Millen Magese group Ltd, Matukio Aranyande Chuma amesema kuwa shindano hili litailetea sifa Tanzania na ni kwa mara ya kwanza kufanyika hivyo wataitumia fursa hiyo kuitangaza nchi kimataifa kupitia urembo.

Kwa upande wake Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye ameahidi kuendelea kufanya mageuzi makubwa katika mashindano ya urembo hapa nchini ili kuondoa dosari zinazojitokeza katika mashindano hayo.

Nape ametoa ahadi hiyo jana Jijini Dar es Salaam wakati akimkabidhi Bendera Mshiriki huyo anayeiwakilisha nchi katika mashindano hayo ya urembo.

Mashindano ya Miss Afrika yameanzishwa mwaka 2016 na Prof. Bena Yage ambaye ni Gavana wa Jimbo la Cross River nchini Nigeria kwa lengo kupata mabalozi wa nchi za Afrika watakaosaidia kutangaza na kuelimisha waafrika kuhusu uchumi unaozingatia utunzaji wa mazingira.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *