Mwenyekiti wa Bodi ya Parole, Agustino Mrema amemwomba Rais John Pombe Magufuli amruhusu kutoa wafungwa wenye sifa ya kupata msamaha.

Mrema amesema kuwa kama wafungwa hao wakitoka kutoka watasaidia kufichua majambazi wanaopora na kuua Polisi.

Pia amesema ana imani majambazi wengi wanaoendesha matukio ya uhalifu wametokea magerezani au watakuwa na uhusiano na wafungwa.

Mrema ametoa ombi hilo baada ya kumalizika kwa msiba wa ndugu yake kijijini kwake Kiraracha Marangu mkoani Kilimanjaro.

Amesema kuwa ipo kampeni mbaya ya kumchafua Rais Magufuli katika utawala wake unaofanywa na wahalifu.

Ameongeza kuwa watu wabaya wasioridhika na uongozi wa Rais Magufuli wanafanya kila mbinu kwa ajili ya kumchafua ikiwemo kufadhili vikundi vya uhalifu vinavyohatarisha amani ya nchi.

Mrema amesema ili kukomesha matukio hayo ni vema Rais akaruhusu bodi yake iwakamate na kuwapunguza wafungwa magerezani hasa wale wenye makosa ya kushindwa kulipa faini ili waweze kufichua wanaohusika na uhalifu huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *