Mwanamuziki maarufu nchini, Mr Nice amekanusha taarifa za kuvamiwa na kuibiwa wakati alipohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Gavana wa jiji la Nairobi nchini Kenya, Sonko.
Sherehe za kuapishwa kwa kiongozi huyo zimefanyika jana jijini Nairobi nchini Kenya ambapo watu mashuhuri waliudhuria sherehe hizo za kuapishwa kiongozi huyo.
Katika sherehe hizo inadaiwa kuwa Mr Nice alivamiwa na vijana wakihuni na kuibiwa baadhi ya vitu vyake, suala ambalo mwanamuziki huyo amelipinga vikali kufanyiwa kitendo hiko.
Kupitia akaunti yake ya Facebook, Mr Nice ameandika kuwa si kweli habari hizo kutokana ajafanyiwa tukio hilo tofauti na baadhi ya waandishi wa habari wanavyosambaza kupitia mitandao ya kijamii.
Mr Nice ameandika kuwa “Kifupi ni kwamba mashabiki waling’ang’ana kucheza na mimi na bahati mbaya wakajikuta wamekata cheni zangu na pia leseni yangu ikadondoka nilikuwa nayo kwa mfuko wa koti la suti,”.
Pia ameongeza “Mkome kabisaaaa kutengeneza ishu za kipumbavu ili muuze vijikaratasi vyenu huko mtaani. Kenya iko sawa na hakuna tatizo lolote kabisaaaaaa na bado 21/8/2017 tuwache rafiki yangu Sonko achape kazi na Nairobi ifaidike naye”.