Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mr Blue amefunguka na kusema toka ameoa mke na kuwa na familia imemsaidia sana kubadili maisha yake na kumfanya aachane na mambo ya kijinga ambayo alikuwa akiyafanya kabla ya kuoa.

Msani huyo amesema hayo baada ya kuulizwa swali na mtangazaji mmoja maarufu nchini kuhusu maisha yake ya sasa ya ndoa na kabla ya kuoa.

Mr Blue amesema kuwa ndoa imemfanya kuwa kijana mwema mwenye kutambua majukumu ya ndoa na kulea familia yake na kuachana na mambo mengine ya hovyo hovyo ambayo alikuwa akiyafanya kabla ya kuoa.

Msanii huyo aliendelea kueleza kuwa wakati yupo kwenye uchumba na mkewe huyo bado alikuwa na mabinti wengine kadhaa ambao alikuwa anatoka nao kimapenzi lakini ilifika hatua aliamua kuoa na kutulia na mkewe wa ndoa.

Kwasasa mwanamuziki huyo ana mke na watoto wawili ambao mmoja mwanamke na mwingine mwanaume.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *