Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Mr Blue amefunguka na kusema kuwa wakati wanaanza kufanya muziki hawakuwaza kufanya hivyo kwa ajili ya kupiga pesa tofauti na ilivyo sasa.
Mr Blue amesema kuwa, siku hizi mtu anatamani kuwa msanii ili apate pesa, lakini kwa upande wa wasanii wa zamani waliwaza kutngeneza ngoma zitakazodumu muda wote hivyo pesa zilikuja zenyewe baadaye.
Amesema kuwa “Siwakatazi wasanii wa sasa hivi kupiga pesa, lakini wakati wetu hatukuwaza kabisa suala la pesa, tuliwaza kutengeneza muziki mzuri utakaoacha alama na pesa zilifuata baadaye.
Pia Mr amesema kuwa tuliamini muziki huu ukishakubalika, pesa zitakuja tu na hivyo ndivyo ilivyokuwa,” anasema Mr Blue; mmoja wa wasanii waliodumu kwenye gemu kwa muda mrefu na ana mafanikio makubwa.