Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mr Blue amefunguka na kusema kuwa yeye na mke wake walikutana Club Bilicanas ndio wakaanza mahusiano yao hadi leo.
Mr Blue amesema kuwa alivyokuwa ameenda Bilicanas kwa ajili ya kazi zake za Kimuziki ndipo alipokutana nae yeye akiwa kwenye Birthday ya Dada yake na Akampenda na kumtuma Baunsa kwenda kumuita Wakaongea.
“Mimi na Mke wangu ni kweli tumekutana Klabu Bilicanas Jumapili mchana yeye alikuwa ameenda kwenye Birthday ya Dada yake na mimi nilienda kwa ajili ya Kazi zangu za kimuziki’ Amesema Mr Blue
Pia ameongeza kwa kusema kuwa hivyo nikampenda nikamtuma Baunsa akamuite, Nikaongea nae tukabadilishana namba na Sasa hivi ni Mke wangu,Mke mzuri sio lazima umpate tu Kanisani”
Mr Blue na mke wake huyo wamejaliwa kupata Watoto wawili wa kike na wakiume na hadi leo wanaishi Pamoja kama mke na mume toka hizo siku za nyuma.