Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga amepiga marufuku kuweka kioo cha giza (tinted) sehemu ya mbele ya gari.
Mpinga amesema sababu ya katazo hilo kwa sababu trafiki wanapata shida kuwaona madereva wanaoendesha magari hayo na pia huwa katika hatari ya kusababisha ajali barabarani.
Mpinga pia amesema kwamba agizo lake kuhusu kuwataka walioweka taa zenye mwanga mkali kwenye magari yao, linahusu taa zote zikiwemo zilizowekwa na wamiliki kama urembo pamoja na zile zilizowekwa kwenye magari hayo viwandani zilizokotengenezwa.
Pia amesema kuwa askari wa usalama barabarani wamekuwa wakipata usumbufu wanaposimamisha magari yenye vioo vya giza mbele kwa kuwa hawamwoni anayeendesha gari.
Ameongeza kwa kusema kuwa askari anamwona anayeendesha gari pale tu dereva anapofungua dirisha.
Amesema kwa sheria za usalama barabarani dereva anatakiwa aonekane hata kama amefunga vioo vya pembeni.