Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) imemhukumu mwanamgambo wa Kiislamu raia wa Mali, Ahmad Al Faqi Al Mahdi kifungo cha miaka tisa jela.

Al-Mahdi ameshtakiwa kwa makosa ya uhalifu wa kivita kuhusiana na kuharibiwa kwa makaburi tisa na msikiti mashuhuri katika mji wa kale wa Timbuktu mnamo mwaka 2012.

Wakati wa kusilikizwa kwa kesi yake, Al Faqi Al Mahdi alikiri mashtaka hayo na kumlazimua kutumikai kifungo.

Kesi dhidi yake ilianzwa kusikizwa siku chache tu kwa sababu yake kukiri makosa yake aliyosemewa na mahakama hiyo.

Al Faqi Al Mahdi ni mwalimu wa kidini na anadaiwa kuamrisha wapiganaji wa kundi la Kiislamu la Ansar Dine waharibu turathi na maeneo ya kidini Timbuktu kati ya 2012 na 2013.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *