Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKIC), Prof. Mohammed Janab ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo August 30, 2017 kuwa moyo wa Mfanyiabiashara Yusuf Manji umewekwa vyuma ili kumsaidia kupumua.

Prof. Janab ambaye ni Daktari wa moyo na Shahidi wa kwanza upande wa uetetezi ameyasema hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha wakati akitoa ushahidi katika kesi ya dawa za kulevya inayomkabili Manji ambapo akiongozwa na Wakili wa utetezi, Hajra Mungula.

Amesema anamfahamu Manji baada ya kufikishwa katika Taasisi hiyo February 2017 akiwa mwenye matatizo ya moyo na kuongeza kuwa alipofikishwa hapo alifanyiwa vipimo na jopo la madaktari lililobaini Moyo wake umewekewa vyuma ambapo akaingizwa mipira maalum na kubaini kwamba upo katika hali nzuri.

Prof. Janab amesema alivyorudi hapo walimpokea kama mgonjwa aliyetibiwa nje ya nchi na ripoti ilionyesha ametibiwa Florida, Marekani.

Prof. Janab ameongeza kuwa katika awamu ya pili ya Manji kurudi hospitalini hapo walimsaidia kumtibia maumivu aliyokuwa nayo kwa kumpa Drip ya Paracetamol’s na Sindano ya Tram a do.

Akijibu hoya ya Wakili wa Serikali, Timony Vitalis kwamba matumizi ya dawa za kulevya yanaweza kusababisha ugonjwa wa moyo, Prof. Janab alijibu ndio.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *