Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ameweka wazi msimamo wake juu ya wachezaji wake wawili, nahodha Wayne Rooney na Ashley Young na kudai ‘hawaondoki’.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mourinho amedai kuwa ingawa magwiji hao wamekuwa wakihusishwa na ligi ya China huku Rooney akihusishwa na mshahara mkubwa zaidi duniani, lakini hawatoondoka kwenye dirisha hili na pia United haitakamilisha mipango ya kumsajili beki Lindelof kutoka Benfica kwa sasa.
‘Young atacheza mechi ya kesho dhidi ya Hull City, anabaki na mimi hadi mwisho wa msimu’. Rooney pia atabaki, hatutouza mchezaji mwingine na wala hatutonunua mchezaji dirisha hili’.
Tayari united imeshawauza wachezaji wawili, Memphis Depay na Morgan Schneiderlin hivyo Mourinho amekataa kuongeza idadi ya wachezaji watakaoondoka Old Trafford Januari hii.
‘Tuko kwenye mashindano ya ligi, tunacheza kombe la FA, tunashiriki Europa na kuna ligi kuu na mechi zinazidi kuongezeka mfululizo hivyo tunamuhitaji kila mchezaji’.
Mustakabali wa nahodha Wayne Rooney na kiungo wa zamani wa aston Villa, Ashley Young umekuwa kwenye tetesi za mijadala mbalimbali ya soka huku wengi waked muda wa mastaa hao kuchezea Old Trafford umefikia tamati.