Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwezi Agosti ligi kuu nchini Uingereza baada ya kuwashinda makocha, Antonio Conte wa Chelsea, Pep Guardiola wa Manchester City na Mike Phelan wa Hull City.
Mourinho ameshinda tuzo hiyo baada ya kukiongoza kikosi cha Manchester United kushinda mechi tatu za ligi kuu nchini Uingereza ambapo wameshinda magoli 6 na kufungwa goli moja tu mpaka sasa.
Kocha huyo amewashinda wapinzani wake wakubwa kwenye kinyang’anyiro hicho baada ya kujizolea kura za kutosha zilizomuwezesha kutwa tuzo hiyo ya kocha bora wa mwezi Agosti nchini Uingereza.
Tuzo hiyo inatoa picha ya mchezo unaofuata kati ya Manchester United chini ya Mourinho na Manchester City chini ya Gurdiola ambapo mchezo huo utachezwa siku ya jumamosi katika dimba la Old Trafford.
Jose Mourinho atataka kuonesha kama tuzo hiyo ameipata kiharali wakati Gurdiola anataka kumuonesha kwamba kupata tuzo hiyo akumaanishi kuwa Mourinho ni bora kuliko yeye kwenye ukocha.
Chama cha Soka nchini Uingereza kinatoa tuzo ya kocha bora kila mwezi pamoja na mchezaji bora ambapo kiungo wa Chelsea na Ubelgiji, Heden Hazard ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Agosti.