Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amewasili katika mahakama ya Uhispania kujibu madai ya kukwepa kulipa kodi wakati alipokuwa kocha wa klabu ya Real Madrid.
Wawakilishi wake wamekana kuwa anadaiwa Euro milioni 3.3 kupitia haki za matangazo ambazo hakuzitangaza.
Mourinho alionekana akiingia mahakamani katika makaazi ya mjini Madrid Pozuelo de Alarcon.
Kusikizwa kwa kesi hiyo kunajiri siku mbili kabla ya Manchester United kucheza dhidi dhidi ya Chelsea katika ligi ya Uingereza.
Utawala wa Uhispania ulianzisha kesi dhidi ya Mourinho mnamo mwezi Juni.