Dansa kutoka kundi la Wasafi Classic Baby (WCB), Moses Iyobo amesema kuwa hajawahi kufikiria kuimba kutokana na kazi hiyo kutumia akili nyingi tofauti na kucheza.

Iyobo amesema ataendelea kubaki kuwa mnenguaji katika maisha yake yote sambamba na kuwa mwalimu kwa wenzake.

Mose Iyobo ambaye ni mzazi na mpenzi wa muigizaji wa Bongo Movie, Aunty Ezekiel amesema kazi ya kuimba inahitaji akili nyingi ili kufikia malengo hivyo ataendelea kubaki na kazi yake ya uchezaji.

Mose amesema kuwa “Nitabaki kuwa dansa maisha yangu yote, labda nitakachoongeza hapo ni kuwa mwalimu na kuwafundisha wengine, unajua kuimba kunahitaji akili nyingi ili ufanikiwe. Sasa kwa upande wangu sitaweza ni bora nibaki huku huku ndio pananifaa zaidi.

Dansa huyo ambaye ni kiongozi wa madansa wa WCB amesema kuwa kazi yake ya unenguaji ni nzuri kwasababu ndiyo imemtambulishwa kwa mashabiki wake kutokana na umahiri wake katika suala zima la kucheza.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *