Naibu waziri Mambo ya Nje wa Morocco, Nasser Bourita amesema kuwa taifa lake halitatambua uhuru wa Sahara ya Magharibi na kwamba atayarai mataifa yanayofanya hivyo kubadili misimamo yao.

Naibu waziri huyo ametoa matamshi hayo katika mahojiano na tuvuti ya Kifaransa ya taifa hilo, Le Desk.

Matamashi yake yanajiri chini ya juma moja tu baada ya taifa la Morocco kurudishwa katika Umoja wa Afrika baada ya kuondoka katika Umoja huo 1984 kufuatia mzozo wa eneo hilo.

Bw Bourita amesema kuwa uanachama wa AU hautabadili msimamo wa Morocco kwamba jimbo la Sahara ya Magharibi ni eneo muhimu la taifa hilo.

Umoja wa Afrika unalitambua eneo hilo kuwa huru na alipo chini ya Morocco licha ya taifa hilo kutotambua uhuru huo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *