Muigizaji wa Bongo Movie, Monalisa amefunguka na kusema jina lake hilo la uigizaji alipewa na muigizaji mwenzake Single Mtambalike maarufu kama Richie Rich.
Monalisa amesema kuwa jina hilo lilikuja siku ambayo ameenda kufanya usaili katika kundi la Mambo Hayo na Mama yake mzazi ndiye aliyempendekeza kwenye kundi hilo.
Jina lake kamili ni Yvonne Cherie, anasema “Namshukuru Mama yangu kwa jina langu alilonipa. Majina yangu ni Yvonne Cherie.
Amesema kuwa Jina la Cherie ni jina langu mimi na nilipewa na Babu yangu. Na Mama alinipa jina la Yvonne kutokana na yeye kumpenda Yvonne Chakachaka.