Muigizaji wa Bongo Movie, Monalisa amefunguka na kusema kuwa anajivunia kuwa muigizaji mkongwe nchini baada ya kufikisha miaka 21 ya uigizaji.
Amesema kuwa ‘Nilianza kujulikana na Watanzania miaka 21 iliyopita kama Muigizaji nikiwa na umri wa miaka 19 kama umri huu alionao sasa binti yangu Sonia.
Haikuwa safari rahisi ya kuishi kama Monalisa kwa zaidi ya Miongo miwili kama watu wanavyodhani, lakini nashukuru kwamba nimeweza kumtenganisha Monalisa na Yvonne.”
Filamu yangu ya kwanza GIRLFRIEND niliigiza huku nikiwa namnyonyesha binti huyu akiwa mchanga kabisa. Look at us now!! Twinning!! Hakika SIKU HAZIGANDI.
Pia amesema kuwa Kesho ndugu zangu rasmi naingia floor ya 4.Huwezi amini, tofauti na wanawake wengi ambao wanaogopa ukubwa, mimi nina furaha mno kuiona siku hiyo ya kesho.