Muigizaji wa Bongo Movie, Yvonne Cherry maarufu kama Monalisa ameweka wazi kuwa hana bifu na msanii mwenzake Kajala Masanja bali watu wanataka kuwagombanisha.
Monalisa amesema watu wamekuwa wakizungumza maneno mengi ambayo yanaweza kusababisha wagombane wakati wao wako vizuri, hawana tofauti yoyote kama watu wanavyosema.
Muigizaji huyo amesema kuwa hana bifu na Kajala ila anaona watu ndiyo wanataka kuwagombanisha baada ya matokeo ya kidato cha nne kutoka ambapo watoto walisoma shule moja na matokeo kuwa mabaya kwa mtoto wa Kajala.
Monalisa amewataka watu waache maneno ya kuwagombanisha ili maisha mengine yaendelee maana wanataka kuwagombanisha.
Monalisa amesema baada ya sakata la matokeo ya kidato cha nne yaliyotoka Wiki chache zilizopita ambapo watoto wa wasanii hao walikuwa wanasoma shule moja lakini baada ya Mtoto wa Kajala Kufeli na Mtoto wa Monalisa kufaulu kuna maneno ya uchochezi yalizungumzwa kupelekea kuonekana kama wana bifu.