Mfanyabiashara na mwanasiasa milionea wa Congo – DRC, Moise Katumbi ameahidi kurejea nyumbani kusindikiza mwili wa mwanasiasa wa upinzani, Etienne Tshisekedi .
Katumbi aliyepo uhamishoni baada ya kukimbia nchini Congo kufuatia kesi za rushwa zinazomkabili ambazo hata hivyo wadadisi wa siasa wanadai kesi hizo zimefunguliwa ili kummaliza kisiasa, ameweka wazi kuwa Tshisekedi anastahili kuzikwa kwa heshima kubwa na yeye angependa kuwa kumbukumbu ya kiongozi huyo nguli wa upinzani.
Bw. Etienne Tshisekedi alifariki dunia mweiz uliopita nchi Ubelgiji alikopelekwa kwaajili ya matibabu.
Bado kumekuwa na mvutano baina ya serikali na vyama vya upinzani juu ya mazishi ya Tshisekedi na mpaka sasa hakuna tarehe rasmi wala mahala pa maziko ambako pamewekwa wazi.
Huenda Katumbi akakabiliwa na kifungo cha miaka mitatu gerezani alichohukumiwa mwezi Juni mwaka jana ingawa hakuwepo mahakani wakati wa kutolewa kwa hukumu hiyo.
Katumbi ndiye mmiliki wa timu, TP Mazembe ya nchini humo.