Mwanamitindo maarufu Bongo, Hamisa Mobetto amewachana watu wote wasiopenda Mahusiano yake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.
Hamisa na Diamond wamerudiana penzi lao rasmi na inaonekana wazi kabisa hivi sasa mambo ni moto kwani Diamond ameonekana ana ukaribu sana na mtoto wao Dylan tofauti na ilivyokuwa siku za nyuma.
Lakini tangu wamerudiana Kumekuwa na maneno mengi yanayosemwa ikiwemo na Mama Diamond kumkataa Hamisa na hata baadhi ya mashabiki kumtolea maneno ya kejeli Hamisa na Diamond.
Hamisa amewaumbua watu wote wasiopenda Mahusiano yao ambapo Kwenye mahojiano na Dizzim Online, Hamisa amesema maneno hayawssumbui kwani ndio wapo wote hivyo.
Hamisa amesema kuwa watu wanachukia yeye kuwa katika mahusiano na Diamond Platnumz kutokana na kuaribu mahusiano ya Diamond na Zari.