Mwanamitindo wa Bongo Fleva, Hamisa Mobeto amefunguka kuwa, kamwe hawezi kumshauri mtu yeyote juu ya uhusiano wake wa kimapenzi kwa sababu hata yeye alishauriwa na wengi, lakini haikwenda hivyo.
Hamisa anasema kuwa, katika mambo ya uhusiano wa kimapenzi ni vigumu kumshauri mtu hata siku moja kwa sababu hata yeye alipokuwa kwenye mapenzi walijitokeza watu mbalimbali na kumshauri, lakini hakuwaelewa, badala yake akaendelea na mambo yake.
“Kwenye mapenzi siwezi kumshauri mtu yeyote hata rafiki yangu wa damu maana ni jambo ambalo ni gumu kumwambia mtu akakuelewa kwa sababu hata mimi walijaribu kunishauri nilipokuwa kwenye uhusiano wangu”.
Pia amesema kuwa ilishindikana mpaka mwenyewe nilipoamua kufanya uamuzi wangu,” anasema Hamisa ambaye aliwahi kuwa kwenye uhusiano na kuzaa na DJ Majizo na Diamond Platnumz.