Mwanamitindo Hamisa Mobetto amesema kuwa anatarajia kufungua duka lake la kuuza nguo hivi karibuni.
Mobeto amunguka kupitia akaunti yake ya Instagram kwa kuwajulisha mashabiki wake ujio a duka hilo.
Hamisa mara baada ya kujifungua mtoto wa Diamond miezi mitatu iliyopita, Hamisa na Diamond waliingia katika mgogoro ambao ulipelekea Diamond kukataa kutoa pesa kwa ajili ya kumuhudumia mtoto kitu kilichomsukuma Hamisa kutafuta wakili wa kumwakilisha na kuenda kumfungulia kesi ya madai Diamond Mahakamani Kisutu.
Siku ya Ijumaa iliyopita kesi hiyo ilitupiliwa mbali na hakimu mkazi Kisutu kwa kile kilichodaiwa kuwa ni makosa katika hati ya awali ya mashtaka ambapo wakili wa Mobetto, Good luck Walter alidai kuwa karani wao alikosea kuchapa hati hiyo ikiwa ni kosa la kibinadamu kabisa.
Kwa kipindi kirefu mashabiki wamekuwa wakimtupia vijembe Hamisa kuwa ni mwanamke asiyetaka kujishughulisha kuwa hana kitu hana biashara yoyote zaidi ya kutegemea matunzo kutoka kwa baba za watoto wake Majizzo na Diamond.
Lakini mapema wiki hii kupitia ukurasa wake wa instagram tayari Hamisa amefunguka na kudai kuwa Ana mpango wa kufungua duka lake hilo la nguo na pia amekataa tuhuma alizokuwa anarushiwa kuwa amejibweteka tu kwani tayari ana biashara zake tangu siku nyingi ambazo watu wengi hawazijui.