Mwanamitindo wa Bongo, Hamisa Mobeto amefunguka sababu inayompelekea asisheherekee siku ya Valentine’s Day leo.
Hamisa amekiri kuwa hawezi kusheherekea siku hiyo kama watu wengine kwasababu inamkumbusha machungu mengi kwasababu siku kama ya leo alifiwa na baba yake mzazi hivyo huwa inamkubusha maumivu.
Pia amesema kuwa hawezi tena kusheherekea siku hiyo kama hapo awali kwa kuwa inamkumbusha mbali kutokana na kifo cha baba yake mzazi kilichotokea tarehe 14 Februari.
Leo ni siku ya Valentine’s Day dunia nzima inasheherekea siku hiyo wakidumisha upendo dhidi ya wapendwa wao.