Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania, Mohammed Dewji amefanikiwa kuingia orodha ya 20 bora ya matajiri barani Afrika kutokana na biashara zake.
Orodha hiyo imetolea na Jarida la Forbes kulingana na uchunguzi uliofanywa na jarida hilo kuhusu matajiri duniani.
Mohamed Dewji ni afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya METL iliyoanzishwa na babake miaka ya 1970.
Kampuni hiyo inahusika katika biashara ya nguo, unga, vinywaji na mafuta mbapo inasambaza ndani na nje ya nchi.
Kampuni hiyo huendesha shughuli zake zaidi ya mataifa sita barani Afrika ambapo bidhaa zake usambazwa.
Orodha ya matajiri 20 bora Afrika
- Aliko Dangote, Nigeria
Utajiri: $12.2 bilioni
- Nicky Oppenheimer, Afrika Kusini
Utajiri: $7 bilioni
- Mike Adenuga, Nigeria
Utajiri: $6.1 bilioni
- Johann Rupert, Afrika Kusini
Utajiri: $6.3 bilioni
- Nassef Sawiris, Misri
Utajiri: $6.2 bilioni
- Christoffel Wiese, Afrika Kusini
Utajiri: $5.9 bilioni
- Nathan Kirsch, Swaziland
Utajiri: $3.9 bilioni
- Naguib Sawiris, Misri
Utajiri: $3.8 bilioni
- Isabel dos Santos, Angola
Utajiri: $3.1 bilioni
- Issad Rebrab, Algeria
Utajiri: $3 bilioni
- Mohamed Mansour, Misri
Utajiri: $2.7 bilioni
- Koos Bekker, Afrika Kusini
Utajiri: $2.1 bilioni
- Allan Gray, Afrika Kusini
Utajiri: $1.99 bilioni
- Othman Benjelloun, Morocco
Utajiri: $1.9 bilioni
- Mohamed Al Fayed, Misri
Utajiri: $1.82 bilioni
- Patrice Motsepe, Afrika Kusini
Utajiri: $1.81 bilioni
- Yasseen Mansour, Misri
Utajiri: $1.76 bilioni
- Folorunsho Alakija, Nigeria
Utajiri: $1.61 bilioni
- Aziz Akhannouch, Morocco
Utajiri: $1.58 bilioni
- Mohammed Dewji, Tanzania