Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited na kukubaliana.
Katika mauzungumzo yao, Rais Magufuli amekubaliana na Mwenyekiti huyo na kusema kuwa wamekubali kulipa fedha ambazo nchi imepoteza kutokana na kampuni hiyo kuendesha shughuli zake hapa nchini.