Mwanzilishi wa mtandao wa Facebook, Mark Zuckerberg kwa mara ya kwanza tangu kuzuka kwa kashfa ya Cambridge Analytica ameibuka na kudai kwamba wamefanya makosa.

Amesema kuwa ni kweli Analytica inatuhumiwa kuingilia data za watumiaji million 50 wa mtandao wa Facebook.

Katika ujumbe wake kupitia ukurasa wake wa Facebook Zuckerberg amesema kitendo hicho kimewavunjia uaminifu. Hivyo kutokana na hali hiyo ameahidi kufanyika mabadiliko kadhaa ili kutoingiliwa na kuibwa kwa taarifa za watumiaji wake.

Amesema kuwa Tuna wajibu wa kuzilinda taarifa zenu,na kama tukishindwa kuzilinda hatuna sifa ya kuwahudumia,mimi ndiye niliyeanzisha mtandao huu wa Facebook,mwisho wa siku nina wajibika kwa chochote kinachotokea katika mtandao wetu.

Mchambuzi wa BBC wa masuala ya kimitandao Dave Lee, BBC kutoka America Kaskazini,anasema kwamba kile anacho kiona ni Facebook kwamba hawapo tayari kuomba radhi kwa kile kilichotokea.

Na pia amesema hakuna maelezo yoyote kwa wizi wa taarifa zake uliofanyika mwaka 2014,hapo ilikuwa ni wakati muafaka kuchukua hatua sitahiki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *