Muigizaji wa Bongo Movie, Yusuf Mlela amefunguka na kusema kuwa bado hajamuona mwanamke wa kumshawishi kuoa hadi pale Mungu atakapomuonesha.
Kauli hiyo hiyo ya Mlela inafuatia baada ya kukaa kwa muda bila kuoa wakati umri wake unakwenda mpaka kupelekea watu kujaji kwanii hadi sasa hivi msanii hajaoa.
Mlela alisema kuoa ni kudra za Mwenyezi Mungu, akipatikana wa kuoa ataoa ila kwa sasa bado hajampata kwa kuwa kila anayemtazama hana vigezo wala sifa.
Amesema kuwa “Kuoa ni kudra za Mwenyezi Mungu, wakati wangu ukifika na nikampata mwanamke wa kuoa itapendeza, nitaoa ila kwa sasa bado naendelea kumtafuta, nikipata mwanamke yeyote anayejua thamani ya mume na anayejiheshimu nitamuoa,”.
Muigizaji huyo amesema kuwa Mungu akimjalia ataoa lakini kwasasa bado kwani hajaona mwanamke wa kumuoa licha ya kuwa kwenye mahusiano.