Katibu Mkuu wa Yanga SC,  Charles Boniface Mkwasa amekanusha taarifa kwamba klabu hiyo inatarajia kuwaacha baadhi ya wachezaji wake.

Hayo yamejiri baada ya taarifa kuendelea kusambazwa katika mitandao ya kijamii kwamba wana nia ya kuwaacha baadhi ya wachezaji wake.

Mkwasa amsema hizo taarifa ni za uzushi ndani ya klabu yao kwasababu hawana nia ya kuwaacha wachezaji wake.

Mkwasa amebainisha hayo kupitia taarifa yake aliyoitoa asubuhi ya leo baada ya kuenea kwa taarifa kutoka baadhi ya vituo vya Radio na ‘social network’ zikidai klabu hiyo inataka kuwabwaga baadhi ya wachezaji wake kutokana na kufanya vibaya katika Ligi.

Aidha, Mkwasa alisisitiza kwamba Kocha Mkuu, George Lwandamina ndiyo mwenye maamuzi ya mwisho juu ya huduma ya wachezaji ndani ya klabu hiyo na wala siyo kiongozi mwingine yoyote

Mkwasa ametumia furasa hiyo kuwahasa mashabiki wa klabu hiyo kuiunga klabu hiyo ili waweze kushinda michezo yao iliyobaki na kushinda taji la ligi kuu Tanzania Bara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *