Katibu Mkuu wa  Yanga, Charles Mkwasa amethibitisha kwamba timu hiyo haitoongeza mchezaji mwingine kwa masaa yaliyobaki ya dirisha dogo la usajili baada ya kumsajili Yohana Mkomola pamoja na  beki Festo Kayembe kutoka Balende FC ya DRC.

Wachezaji hao walisajiliwa mapema mwezi uliopita baada ya dirisha la usajili kufunguliwa, huku akisema kwamba  isingekuwa tatizo la  majeruhi ya baadhi ya wachezaji wao muhimu wasinge sajili hadi dirisha kubwa la usajili.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi kuu Tanzania bara wanajiandaa na mashindano ya Mapinduzi pamoja na kombe la Shirikisho huku hatua ya 12 ikisubiriwa kwa hamu na wapenzi  wa mpira wa miguu.

”Ni kweli tumefanya baadhi ya usajili tatizo likiwa majeruhi ya mara kwa mara kwa wachezaji wetu muhimu, labda wasingekuwa majeruhi tusinge sajili,” amesema.

Dirisha dogo la usajili linafungwa Desemba 23 saa sita usiku. Wakati watoto wa Jangwani wakimaliza hatua ya usajili bado watani wao wa jadi Simba  wanahangaika na beki wa Lipuli Asante Kwasi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *