Mkutano wa nne wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeanza leo mjini Dodoma huku miswada sita ukiwemo wa sheria ya upatikanaji wa habari ukitarajiwa kuchukua nafasi kubwa zaidi.
Kwa mujibu wa taarifa ya kitengo cha habari na mawasiliano ya bunge miswada sita ya sheria iliyosomwa kwa mara ya kwanza katika mkutano wa tatu wa bunge na baadaye kupelekwa katika kamati husika ili ifanyiwe kazi itajadiliwa.
Miswada hiyo ni pamoja ule wa sheria ya upatikanaji wa habari ya mwaka 2015, muswada wa sheria ya utathmini na usajili wa wathamini wa mwaka 2016, muswada wa sheria ya mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu wa serikali wa mwaka 2016
Taarifa hiyo imeongeza kuwa pia kutakuwa na musadwa wa sheria ya usimamizi wa wanataaluma wa kemia wa mwaka 2016, muswada wa sheria ya taaasisi ya utafiti wa kilimo wa mwaka 2016 na muswada wa sheria ya taasisi ya utafiti wa uvuvi ya mwaka 2016.