Jeshi la Polisi Mkoani Tanga limezuiya Ziara ya Mwenyekiti wa Kamati ya uongozi wa Chama Cha CUF Juliasi Mtatiro.

Mtatiro  aliwasili jijini Tanga jana jioni kwa lengo la kufanya vikao vya ndani pamoja na kufungua matawi  kazi ambayo ilikuwa aifanye leo na kesho.

Mwenyekiti wa CUF ,Wilaya ya Tanga, Rashid Jumbe amesema licha ya
kwamba hadi jana jioni walikuwa na barua kutoka jeshi la polisi ya
kuwaruhusu kuendelea na ziara ya Mtatiro lakini leo saa 3.00 asubuhi
walizuiwa.

Mwenyekiti  huyo alieleza kushangazwa kwake na kitendo cha jeshi la
polisi kufanyia kazi maelekezo ya Sakaya huku akisisitiza kwamba CUF
Tanga haimtambui  kwa sababu alishafukuzwa uanachama.

Amesema Julias Mtatiro alikuwa amepangiwa  kukutana na viongozi wa
kamati ya utendaji ya Wilaya ya Tanga, madiwani, wabunge, kufungua matawi
ya Kata ya Duga, Masiwani Shamba, Masiwani, Mabawa, Magaoni, Mnyanjani, Pongwe na Kwanjeka.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba amesema
wamezuia ziara hiyo kufuatia jeshi la polisi kupokea  barua mbili
tofauti zenye kupingana jambo lililoashiria kuwa kusingekuwa na amani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *