Mkutano wa chama cha Jubilee nchini Kenya umeshindwa kuendelea katika kaunti ya Taita – Taveta baada ya kuvamiwa na nyuki.

Wafuasi wa chama hicho walilazimika kukimbilia usalama wao wakati nyuki hao walipowavamia , lakini wakapotea baada ya maombi kufanywa na mwanasiasa mmoja.

Wanasiasa walilaumu shetani kwa uvamizi huo wa mkutano huo uliofanyika katika mji wa Wundanyi ,ulioitishwa kumuunga mkono rais Uhuru Kenyatta kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio wa Oktoba 26.

Mahakama ya juu nchini humo ilifutilia mbali ushindi wa rais Uhuru Kenyatta dhidi ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga mnamo tarehe 8 mwezi Agosti ikisema kuwa uchaguzi huo ulikuwa na mkosa chungu nzima ikiwemo udanganyifu.

Nyuki wengine waliwavamia maafisa wa polisi na watu wengine nje ya mahakama katika mji mkuu wa Nairobi , wakati majaji walipotoa uamuzi wao kamili kuhusu kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi huo tarehe 20 mwezi Agosti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *