Mkutano mkuu wa FIFa wa Mwaka utakashirikisha mataifa 19 utarajia kufanyika Tanzania Februari 22 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa mkutano huo, Rais wa FIFA Gianni Infantino, Katibu Mkuu wa FIFA, Fatma Samba Diouf Samoura na Sekretarieti ya FIFA pamoja na rais wa CAF, Ahmad Ahmad na Sekreterieti yake, ni miongoni mwa wageni wa ngazi ya juu watakaohudhuria.

Agenda kadhaa zitakazojadiliwa ni pamoja na utoaji wa Fedha za FIFA kwaajili ya maendeleo ya mchezo wa soka, changamoto za usajili wa wachezaji kwa kutumia mtandao yaani TRANSFER MATCHING SYSTEM na kalenda ya kimataifa ya FIFA.

Baadhi ya nchi zitakazoshiriki katika mkutano huo ni Bahran, Saudi Arabia, Palestina, Algeria, , Ivory Coast, Tunisia, Mali na Niger.

Hii ni kwa mara ya kwanza kwa mkutano mkubwa wa Fifa kufanyika nchini Tanzania toka aingie madarakani Rais mpya wa TFF, Karia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *