Mkurugenzi wa kampuni ya Ringing Bells, inayouza bei simu za bei nafuu nchini India, Mohit Goel amekamatwa kwa madai ya ulghai.

Mohit Goel amekamatwa baada ya kampuni moja inayosambaza simu hizo kwa wauzaji kudai kwamba ilikuwa haijapokea simu ambazo ilikuwa imelipia.

Simu hiyo ya Freedom 251, ambayo bei yake ni rupia 251 ($3.70; £3), ilianza kuuzwa Februari 2016.

Lakini ingawa wateja wengi walipokea simu walizoagiza, Ringing Bells imedaiwa kutotimiza maombi yote ya ununuzi wa simu hizo.

Kampuni ya Ayam Enterprises, imesema ililipa rupia 3m ($45,000; £35,800) baada ya Bw Goel kuishawishi ifanye biashara ya kusambaza simu hizo.

Lakini inadai ilipokea simu za thamani ya rupia 1.4m pekee na wafanyakazi wake walitishiwa walipodai “pesa tena na tena”.

Msemaji wa polisi Rahul Srivastava amethibitishia kuwa Bwana Goel amekamatwa na atafikishwa mahakamani leo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *