Mkimbizi wa Syria, Ninorta Bahno ameshida taji la ‘Umalkia’ na kampuni moja ya kutengeneza mvinyo Ujerumani na kuwa mkimbizi wa kwanza kupokea taji hilo.
Ninorta Bahno mwenye umri wa miaka 26 ni mwanafunzi ameitoroka Syria zaidi ya miaka mitatu iliyopita.
MSyria huyo mkristo alizawadia tuzo hilo huko mjini Trier, magharibi mwa Ujerumani, katika eneo la Moselle karibu na mpaka na Luxembourg , ambalo linajulikana sana kwa kutengeneza mvinyo.
Ninorta Bahno asema anatumai taji hilo litasaidia kuleta utengamano baina ya raia wa ujerumani na wakimbizi wanaotafuta hifadhi nchini humo kama yeye.
Mwaka jana Ujerumani ilipokea wakimbizi zaidi ya millioni moja igrants, wengi wao kutoka Syria.
Bahno atakuwa akiwawakilisha watengezaji mvinyo wa eneo hilo katika tamasha mbalimbali za huko Trier huku akisema baadhi ya wakimbizi aliozungumza nao wamefurahiya na kumpongeza kwa kushinda taji hilo.
Bahno amesema ilimbidi kufanya mafunzo ya dharura ya jinsi ya kutengeneza mvinyo na anapendelea ule iitwayo sweet Riesling.
Taji hiyo la Malkia wa Ujerumani ilianza tangu 1930 na ushirikisha jumla ya majimbo 13 ya Ujerumani hushiriki kuwania taji hilo la ‘The German Wine Queen’.