Mke wa rais wa Zimbabwe, Roberto Mugabe aitwae Grace Mugabe ametakiwa na jaji wa mahakama nchini humo kurudisha nyumba tatu alizompokonya mfanyabiashara nmoja raia wa Lebanon kufuatia zabuni ya pete ya almasi ya gharama ya dola milioni 1.35.

Kulingana na kesi iliyowasilishwa na mfanyabiashara huyo, mke huyo wa Mugabe ametaka kurudishiwa pesa baada ya pete hiyo ya almasi iliyonunuliwa mjini Dubai.

Mfanyabiashara huyo, Jamal Ahmed alishindwa kulipa pesa hizo kwa akaunti ya Dubai, na licha ya yeye kusema kuwa pesa hizo zilitumwa kupitia kwa benki moja ya Zimbabwe, Bi Mugabe alichukua kwa nguvu nyumba zake tatu mwezi Oktoba.

Jaji Clement Phiri amesema kuwa Bi Mugabe pia ni lazima ahakikishe kuwa wafanyakazi wote waliokuwa wakihudumu kwenye nyumba hizo wamerudishwa kazini.

Pete hiyo ilikuwa ni kama zawadi kwa mke wa rais Mugabe, Bi Grace, kuadhimisha miaka 20 ya ndoa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *