Mbunge wa upinzani nchini Zimbabwe Eddie Cross amesema kuwa anaamini mke wa Rais Mugabe, Grace, ametorokea Namibia.

Mwanasiasa huyo wa chama cha Movement for Democratic Change (MDC) amesema anafahamu kwamba Grace aliruhusiwa kuondoka nchini humo usiku wa kuamkia leo na jeshi.

Ameongeza kwamba alikuwa hana kwingi kwa kwenda kutafuta hifadhi baada yake kudaiwa kumdhalilisha mwanamitindo Afrika Kusini jambo lililomaanisha kwamba hawezi kuwa salama huko.

Kwenye taarifa rasmi kwenye runinga ya taifa awali, Meja Jenerali Sibusiso Moyo alihakikishia taifa hilo kwamba rais na familia yake walikuwa salama na usalama wao ulikuwa umehakikishwa.

Taarifa hiyo ilionekana kuashiria kwamba huenda familia ya rais ilikuwa inazuiliwa kwa pamoja nyumbani kwao Harare.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *