Mke wa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, Bi Aisha Buhari amesema kuwa mumewe huyo anaendelea vizuri na matibabu nchini Uingereza.
Mke huyo wa Rais amaesema hayo, baada ya kuzuru London, mahali ambapo mumewe anaendelea na matibabu kutokana na ugonjwa ambao bado haujatajwa.
Buhari mwenye umria wa mia 74 alipelekwa hospitalini jijini London mwezi mmoja uliopita, kwa ziara yake ya pili ya matibabu nchini Uingereza mwaka huu.
Kukosekana kwake nchini Nigeria kumesababisha mihemko nchini Nigeria, taifa lenye uchumi mkubwa na idadi kubwa ya watu barani Afrika, huku baadhi ya watu wakiteta kuhusiana na iwapo ataweza kurejelea kazi yake tena.
Naibu wa Rais Yemi Osinbajo anatumika kama kaimu, na amesifiwa pakubwa kwa namna anavyoshughulikia mzozo wa kiuchumi, hasa baada ya kushuka kwa bei ya mafuta, bidhaa muhimu inayouzwa kwa wingi nje ya nchi.
Mwezi Januari mwaka huu, Bwana Buhari alichukua wiki saba ya likizo ya matibabu kwenda Uingereza.
Aliporejea nyumbani mwezi Machi, alisema kuwa ameongezewa damu, lakini hakufichua ni ugonjwa gani anaougua.
Alirejea tena Uingereza mnamo Mei 7, kwa matibabu zaidi jijini London nchini Uingereza kwa ajili ya matibabu zaidi.