Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa amezindua nyumba ya wahudumu wa afya katika kijiji cha Mkungo wilayani Chato mkoani Geita zilizojengwa na taasisi ya Mkapa Foundation kwa kushirikiana na Serikali.

Akizindua nyumba hizo jana, Rais Mkapa amewataka wananchi wa mkoa huo kutunza nyumba hizo na kushirikiana vema na watumishi watakaoshi katika nyumba hizo.

Mkapa aliingia katika eneo la zahanati hiyo saa sita mchana akiongozana na mkewe, Mama Anna Mkapa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.

Uzinduzi wa nyumba hiyo ni ishara ya kuzindua nyumba nyingine 50 zilizopo katika mikoa ya Geita, Simuyu na Kagera .

Makabidhiano ya nyumba hizo yanatarajiwa kufanyika leo katika uwanja wa mpira wa miguu uliopo Chato mjini hafla itakayohudhuriwa na Rais John Magufuli.

Ofisa Mahusiano na Mawasiliano wa Mkapa Foundation, Deogratius Rimoy alisema nyumba 50 zilizojengwa na taasisi hiyo katika mikoa mitatu tofauti zimegharimu kiasi cha Sh bilioni 2.5.

Amesema lengo la kujenga nyumba hizo ni ili kuboresha huduma za afya vijijini illi watumishi waweze kutoa huduma za afya kwa saa 24.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *