Mwanamuziki wa wimbo wa Songi Songi, Maud Elka, anatarajia kutua Bongo, Oktoba 5 mwaka huu.
Hayo yameelezwa na msanii wa Bongo Fleva, Alikiba alipokuwa akizungumzia ujio wa albamu yake mpya,anayotarajia kuiachia Oktoba 7 mwaka huu.
AliKiba na Maud walifanya remix ya wimbo wa Songi Songi na kuutoa Julai.Kabla ya hapo wimbo huo uliotoka miezi sita iliyopita ambapo msanii huyu kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo alimshirikisha Hiro.
Katika mkutano wake huo na waandshi wa habari leo, Alikiba alilolulizwa ni lini haswa ataachia video ya wimbo huo.
Mwandishi alienda mbali na kueleza ni wimbo uliopekelewa vizuri lakini watu wanataka kujua lini haswa video yake itatoka kwani huenda ikafanya vizuri zaidi.
Katika majibu yake Ali Kiba amesema mashabiki watarajie video hivi karibuni na masanii huyo anatua nchini Oktoba 5,ambapo pamoja na shughuli nyingine watarekodi video.
Ukiachilia mbali uzuri wa biti la wimbo huo, umekuwa ukipendwa sana kutokana na namna ya uchezaji wake ambapo wapenzi walikuwa wakishindana kuucheza.