Mtoto wa pili wa rais wa Marekani, Barrack Obama, Sasha Obama ameshindwa kuhuduria sherehe ya kuagwa kwa baba yake kutokana na kukabiliwa na mitihani katika shule ya Sidwell iliyopo jijini Washington.
Picha ya pamoja iliopigwa ilimuonyesha rais Obama, mkewe na mwanawe mkubwa Malia mbele ya jukwaa lakini msichana hyo wa miaka 15 hakuonekana katika maeneo hayo.
Imeelezewa kwamba msichana huyo alikuwa akifanya mtihani katika shule ya Sidwell mapema siku ya Jumatano.
Shule hiyo ndio imewafunza watoto wa marais kwa miaka mingi akiwemo Chelsea Clinton mtoto wa aliyekuwa mgombea urais wa Marekani kwenye uchaguzi mkuu uliopita Bi Hillary Clinton.
Shule hiyo imekuwa ikitumika kukabiliana na wanafunzi ambao wamekuwa wakikosa masomo kutokana na kuhudhuria maswala ya uongozi ya wazazi wao.
Kutokana na kukosekana kwa mtoto huyo watu wakaanza kujiuliza msichana huyo yupo wapi wakaamua kuanzisha hashtag kupitia mitandao ya kijamii iliyokuwa #WhereIsSasha.