Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mimi Mars amesema kuwa sababu kuu ya kuwa anaimba nyimbo za mapenzi mara kwa mara ni kutokana na kuumizwa kimapenzi.
Mimi Mars anakiri amefanya kazi nyingi zinazohusu mapenzi tangu ameanza muziki kwa sababu anapenda mapenzi, lakini yamekuwa yanamuumiza.
“Mimi ni mwanamke, nimeshavuka miaka 18, nilishakuwa kwenye mahusiano na nimeumizwa sana kwenye sekta hiyo, naweza kusema ndiyo sababu ya kufanya kazi nyingi zinazohusu mapenzi,”
Pia amesema kuwa Mimi Mars ambaye hivi karibuni zilisambaa tetesi kwamba anatoka kimapenzi na msanii Marioo huku wenyewe wakitumia nguvu nyingi kukanusha.
Kwa sasa Mimi Mars anafanya vizuri na wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la La La ambao amemshirikisha Marioo.