Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amekiri kuwepo kwa uhaba wa wahudumu wa afya nchini ambapo ametaja mikoa ya Kagera, Katavi, Shinyanga, Ruvuma na Rukwa kuwa inaongoza kwa kuwa na uhaba mkubwa.

Akiongea katika ufunguzi wa Mkutano na Wadau wa Afya kujadili namna ambavyo watakabiliana na uhaba wa wahudumu wa afya, ukosefu wa huduma za dharura na kupunguza vifo vya mama na mtoto.

 

Mhe Ummy amesema serikali inakusudia kupunguza uhaba huo kwa kuongeza wahudumu wa afya mapema mwakani.

 

Mbali na mkutano huo, Mhe. Ummy Mwalimu amepokea magari ya kubeba wagonjwa (Ambulance) 10 kutoka kwa serikali ya Qatar ambayo imewasilishwa na balozi wa nchi hiyo nchi Tanzania Bw. Abdallah Bin Jassim Al medadi ambazo zitatumika kwenye vituo mbalimbali vya afya nchini katika kuhakikisha kuwa kina mama wajawazito wanawahishwa katika vituo vya afya kupata huduma.

 

Naye, Naibu Katibu Mkuu wa Tamisemi Bi. Zainabu Chaula amesema ifikapo mwakani serikali itapeleka fedha za ruzuku na huduma mahosiptalini moja kwa moja na kuachana na utaratibu wa sasa wa kupitisha fedha katika halmashauri ili kuongeza kasi ya upatikanaji wa madawa na huduma bora.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *