Kikosi cha uokozi cha Italia kimefanikiwa kuipata miili ya watu wawili wa mwisho waliokuwa wameangukiwa na kifusi cha theluji kwenye hoteli ya Rigopiano.
Miili hiyo inatimiza idadi ya watu waliokuwa kwenye hoteli hiyo wakati ajali hiyo ilipotokea hivyo kukamilisha zoezi la uokoaji wa watu lililokuwa likiendelea.
Ajali hiyo iliyotokea wiki iliyopita ilipelekea watu kumina namoja kujeruhiwa kati yao wakiwemo watoto wanne waliotolewa kwenye vifusi vya theluji wakiwa hai.
Waziri mkuu wa Italia, Paulo Gentiloni amedai kuwa taarifa za kuwa maafisa usalama wa eneo la ajali hawakuchukua hatua stahiki za uokozi kwa haraka.
Hata hivyo Bunge la Italia limemuomba waziri huyo mkuu kuacha kumtafuta wa kumtupia lawama.
Kifusi hicho cha theluji kinadaiwa kuwa kilikuwa na uzito wa tani 120,000 na kilikuwa na kasi 100km/h (60mph).
Uchunguzi wa miili ya marehemu sita uliofanywa baada ya ajali hiyo unadaiwa kuonyesha ushahidi kuwa watu wengi walikufa kwa kuumizwa sana na mabaki ya jengo hilo ingawa watu wawili pia walikutwa na dalili za kufariki kwa kukosa hewa (asphyxiation) na mwili kukosa joto (hypothermia).
Uchunguzi wa makosa ya jinai tayari umeanza baada ya ripoti kudai kuwa maafisa wa eneo la Pescara kupuuzia simu zilizopigwa na watu wawili walinusurika kwenye ajali hiyo kisha waokoaji kuja baada ya saa kadhaa kupita.
Mmoja wa watu waliopatikana jana ni mwili wa Stefano Feniello mwenye miaka 28.
Wakati wa kutokea kwa ajali hiyo, hoteli hiyo ilikuwa na watu 40 ambapo kati yao 29 wamefariki dunia.