Rais Mpya wa Brazil, Michel Temer amesema nchi yake inaingia katika enzi mpya ya matumaini baada ya kuondoshwa madarakani kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Dilma Rousseff.
Rais Temer ametoa wito wa kuungana pamoja na kusema kuwa kuondolewa madarakani kwa bibi Rousseff kumemaliza miezi kadhaa ya mashaka.
Wabunge nchini humo walipiga kura ya kutokuwa na imani na Bibi Rousseff ya kumuondoa madarakani kwa asilimia 61 huku kura 20, zikipinga kuondolewa kwake.
Amekutwa na hatia ya udanganyifu wa bajeti ya nchi hiyo wakati wa kampeni zake za uchaguzi muiaska miwili iliyopita.
Michel Temer ambaye amemrithi Bi Rousseff kwa muda amekula kiapo cha urais hadi ifikapo January 2019.
Katika majibu yake ya kwanza ya kura zilizopigwa Bi Rousseff amesema kuwa, Baraza la Seneti halikutenda haki kwa mwanamke asiye na hatia.
Bi Rousseff amewashutumu Maseneta ambao walipiga kura ya kumuondoa madarakani kwamba wamehusika katika mapinduzi ya kisiasa.