Aliyekuwa Mhasibu mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na  Kupambana na Rushwa (Takukuru), Godfrey John Gugai amejisalimisha katika taasisi hiyo.

Ayo yamethibitishwa na  Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Kamishna Valentino Mlowola ambapo amesema kuwa Gugai amejisalimisha na hatua za kisheria zinaendelea.

Mtumishi huyo anatuhumiwa kujipatia mali kinyume cha Sheria za Utumishi wa umma huku Takukuru wakidai kwamba kama atadhibitisha uhalali wa umiliki wake ataachiwa na akishindwa atachukuliwa hatua.

Gugai amejisalimisha ikiwa ni siku moja imepita tangu Takukuru ilipotangaza zawadi ya Sh 10 milioni kwa mwananchi yoyote ambaye angefanikisha kumtia nguvuni mtumishi  huyo.

Lakini Kamishna Molowa ameshindwa kufafanua kama amejisalimisha mwenyewe au kuna mtu katoa taarifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *