Mwenyekiti  wa Taasisi ya Tanzania Mzalendo Foundation, Khamis Mgeja amelaani kitendo cha kutishiwa kwa silaha ya moto aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.

Amesema kwamba, kitendo kilichofanyika dhidi ya Nape ni ukiukwaji wa haki za kibinadamu na utawala bora ambacho hakiwezi kuvumiliwa.

Mgeja, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, kabla hajahamia Chadema mwaka juzi, alitoa kauli hiyo jana, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mkoani Kigoma.

Pamoja na hayo amemuomba Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, asimame hadharani kuwaomba radhi Watanzania kwa niaba ya Serikali.

Mgeja amesema kuwa “Mbali ya kuwaomba radhi Watanzania, waziri mkuu achukue hatua mara moja ya kukomesha vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwamo kuheshimu misingi ya demokrasia kwa kuzingatia katiba ya nchi, sheria, kanuni na taratibu,”.

Akifafanua zaidi, mwanasiasa huyo alisema tukio la Nape kutishiwa silaha ni moja ya matukio ya ukandamizaji wa haki za binadamu yanayoendelea kutokea nchini na kwamba yanatakiwa kukemewa kabla hayajaleta madhara zaidi kwa wananchi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *