Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob (Chadema) ameachiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa na polisi kwa takribani saa 15 tangu jana.

Meya huyo anadaiwa kutaka kupanga njama za vurugu baada ya matokeo ya udiwani wa Kata ya Saranga kutangazwa.

Meya Jacob alikuwa wakala katika majumuisho ya uchaguzi wa Kata ya Saranga hivyo alikuwa anahusika katika uchaguzi uliofanyika jana katika kata hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *