Rais wa Mexico, Enrique Pena Nieto amesema kuwa Mexico haitalipia ukuta uliopendekezwa na rais wa Marekani Donald Trump.

Rais huyo pia amesema kuwa atafutilia mbali ziara yake ya Marekani ambapo anatarajiwa kukutana na rais Donald Trump Januari 31 mwaka huu.

Trump tayari amesaini agizo la urais la kujenga ukuta kati ya Marekani na Mexico na amesisitiza kuwa Mexico itailipa Marekani kwa ukuta huo.

Rais Pena Nieto aliambia taifa katika hotuba ya runinga kwamba :Nimesema tena na tena kwamba Mexico haitalipia ukuta huo.

Rais huyo amesema kuwa ”Ninajuta na kushutumu uamuzi huo wa marekani wa kutaka kuendelea kujenga ukuta ambao umetugawanya kwa miaka badala ya kutuunganisha”.

Kwa upande mwingine Rais huyo amesema kuwa urafiki kati ya Mexico na raia wa Marekani utadumu mbali na kutafuta suluhu kuhusu tatizo la wahamiaji.

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Mexico Luis Videgaray ambaye yuko mjini Washington amesema kuwa rais huyo bado anaendelea kupima uwezekano wa ziara ya Marekani siku ya Jumanne lakini akaongezea kuwa mkutano huo bado utafanyika kufikia sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *