Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi ametoa masharti matatu kwa klabu yake ili asaini mkataba mpya na klabu hiyo yenye maskani yake katika jiji la Cataluna nchini Uhispania.
Sharti la kwanza alilotoa Lionel Messi anataka bonasi yake ilingane kama Neymar wakati aliposajiliwa kujinga na Barcelona akitokea Santos ya Brazili mwaka 2013.
Sharti la pili wamlipie deni la kodi analodaiwa na Serikali ya Uhispania baada ya kuhukumiwa kulipa deni hilo kutokana na ukwepaji wa kodi ambapo ni kosa kisheria na sharti la tatu atasaini mkataba mpya mpaka mwaka 2021 huku yeye akiwa mchezaji anayelipwa mkwanja mrefu zaidi kwa kupokea Euro milioni 30 kwa mwaka.
Kutokana na masharti hayo ya Lionel Messi klabu ya Barcelona imekubali masharti hayo na Lionel Messi hivi karibuni ataisani mkataba mpya ili aendelee kubaki kwa mabingwa hao wa Uhispania.